Wakati dirisha la usajili lilipofunguliwa Yanga ilionekana kupoteza mwelekeo hasa baada ya kudaiwa kuwa haina uwezo wa kifedha.
Baadhi ya wachezaji waliokuwa wakiwindwa na timu hiyo waliishia kusajiliwa na timu nyingine kwa mbwembwe.
Lakini sasa kwa yaliyotokea siku mbili zilizopita, ni dhahiri 'neema' imerejea Jangwani. Licha ya kwamba bado hajaonekana klabuni, Mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Manji amerejea rasmi.
Katika muda wa saa 48 Yanga imetangaza kusajili wachezaji watatu Mohammed Issa 'Banka', Feisal Salum na Jaffar Mohammed.
Usajili wa Feisal 'Fei Toto' ndio umekuwa gumzo zaidi kutokana na namna Yanga ilivyomnyakua kiungo huo fundi 'kibabe'.
Mchana klabu ya Singida United ilitangaza kumsajili lakini saa chache baadae Yanga wakaibuka nae kwenye Mkutano na waandishi wa habari kutambulisha usajili wake.
Ili kuondoa sintofahamu, kwenye utambulisho Yanga wakaambatana na viongozi wa JKU pamoja na Meneja wa Feisal.
Feisal pia alikuwa akiwaniwa na Simba ambayo inadaiwa ilimuweka mafichoni juzi baada ya kumalizika kwa mchezo wa kombe la Kagame kati ya Simba dhidi ya JKU.
Lakini Yanga ikauteka mchakato wa usajili asubuhi ya jana kisha kumalizana nae pamoja na JKU.
Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika amesema Yanga ndio imeanza rasmi kusajili na wataendelea kutambulisha wachezaji wapya wiki nzima.

ADVERTISE HERE