Yanayojiri Urusi : Uingereza vs Croatia, nani kwenda fainali?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Jul 2018
Yanayojiri Urusi : Uingereza vs Croatia, nani kwenda fainali?
Baada ya hapo jana Ufaransa kutinga fainali ya michuano ya kombe la dunia kwa kuilaza Ubelgiji bao 1-0, leo itakuwa zamu ya 'watoto wa Malkia' Uingereza ambayo itachuana na Croatia katika mchezo wa pili wa nusu fainali.

Mchezo huo utapigwa kwenye dimba la Luzhniki ukitarajiwa kuanza saa tatu usiku.

Hii itakuwa mara ya nane kwa Uingereza kucheza na Croatia, ambapo imeshinda michezo minne na kupoteza mchezo mmoja pekee.

Lakini pia hii itakuwa mara ya kwanza kwa timu hizo kukutana kwenye michuano ya kombe la dunia.

Mwaka 2004 zilikutana kwenye michuano ya Euro hatua ya makundi na Uingereza kuibuka na ushindi wa mabao 4-2.

Uingereza itakuwa inacheza mchezo wake wa tatu wa nusu fainali ya michuano ya kombe la dunia ambapo mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1966 ilipoifunga Ureno mabao 2-1 na kutinga fainali na kufanikiwa kutwaa taji hilo.

Mwaka 1990 ilifika hatua hiyo lakini ikalazwa kwa matuta na Ujerumani ambayo ilifanikiwa kutwaa taji hilo.

Sasa ni miaka 28 imepita tangu wafikie mafanikio hayo na ndio sababu shamrashamra zimepamba moto nchini Uingereza wengi wakiwa na matumaini makubwa timu yao itashinda mchezo wao na kukutana na Ufaransa kwenye mchezo wa fainali.

Kwa Croatia hii ni mara yao ya pili kucheza nusu fainali baada ya kufanikiwa kufanya hivyo mwaka 1998. Haijawahi kushinda taji la dunia.

Mchezo huo sio rahisi kutabirika kwa kuwa timu zote zimeonyesha kuwa bora katika michuano ya mwaka huu.

Wakati Uingereza ikitegemea makali ya kinara wake wa mabao sita Harry Kane, Croatia imekuwa ikicheza kitimu zaidi.

Croatia ina wachezaji nane tofauti waliofunga mabao kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka huu. Wamezidiwa na Ubelgiji pekee yenye wachezaji tisa.

Mshindi wa mchezo huo ataumana na Ufaransa kwenye mchezo wa fainali Jumapili, Julai 15 wakati timu itakayofungwa itaumana na Ubelgiji kusaka nafasi ya tatu siku ya Jumamosi, Julai 14 2018.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’