Yanayojiri Urusi : Ufaransa yatinga fainali kombe la dunia, yailaza Ubelgiji 1-0

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Jul 2018
Yanayojiri Urusi : Ufaransa yatinga fainali kombe la dunia, yailaza Ubelgiji 1-0
Ufaransa inakaribia kurudia historia ya mwaka 1998 ya kutwaa kombe la dunia baada ya kutinga fainali ya michuano hiyo kwa kuilaza Ubelgiji bao 1-0 katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la St Petersburg, Urusi.

Bao pekee la Ufaransa lililoipeleka timu hiyo fainali lilifungwa kwa kichwa na beki Samuel Umtiti kwenye dakika ya 51.

Wakati Ubelgiji ikimiliki mchezo kwa muda mwingi, Ufaransa ilitumia mbinu ya kujilinda na kushambuliza kwa kushitukiza kupitia washambuliaji wake wenye kasi Kylian Mbappe na Antoine Griezmann.

Licha ya juhudi za Ubelgiji kusaka bao la kusawazisha wakiongozwa na nahodha wao Eden Hazard, walishindwa kuipenya ngome ya Ufaransa huku mlinda lango wa timu hiyo Hugo lloris akiweza kudhibiti michomo ya mbali iliyoachiwa na wachezaji wa Ubelgiji.

Ufaransa sasa inasubiri mshindi wa mchezo kati ya Uingereza dhidi ya Croatia kwa ajili ya mchezo wa fainali utakaopigwa Jumapili ijayo, Juni 15.

Ubelgiji itacheza na timu itakayofungwa kusaka mshindi wa tatu Jumamosi, Juni 14
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’