Mwenyekiti wa Matawi Yanga amjia juu Tarimba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Jul 2018
Mwenyekiti wa Matawi Yanga amjia juu Tarimba
Mwenyekiti wa Matawi ya klabu ya Yanga nchini Bakili Makele amemjia juu aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Mpito Abbas Tarimba kwa kuzungumza mambo yanayoihusu klabu hiyo nje kinyume na utaratibu.

Makele amewaambia waandishi wa Habari leo Makao Makuu ya Yanga Jangwani jijini Dar es salaam kuwa kitendo alichokifanya Tarimba sio cha kiungwana na ameonyesha hana mapenzi na klabu hiyo.

Makele amekanusha taarifa zilizotolewa na Tarimba juu ya kuvunjwa kwa Kamati Maalum ya Mpito akieleza kuwa hazikuwa za kweli.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga hakuvunja Kamati hiyo kwa kuwa hana Mamlaka ya kufanya hivyo.

Amedai walimualika Sanga kwenye Mkutano wa Wenyeviti wa Matawi ili aweze kutoa taarifa juu ya nini kinaendelea klabuni hasa ikizingatiwa Yanga inakabiliwa na mchezo dhidi ya Gor Mahia wiki ijayo, pamoja na masuala ya usajili wakati huu dirisha la usajili likielekea ukingoni.

Makele amesema Sanga aliwahakikishia kuwa tangu ateuliwe kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mpito, Tarimba hajaisaidia Yanga kwa jambo lolote.

"Tangu ameteuliwa hajawahi kufanya jambo lolote katika klabu yetu, sasa anapoenda kulalamika na kuungana na watu ambao hawapo na sisi jambo hilo ni baya kwetu na inaonekana hana mapenzi na sisi licha ya kwamba alikuwa ni kiongozi katika klabu,"amesema.

"Sisi tuna mkataba na SportPesa kama ambavyo ilivyo vilabu vingine, hatutumii pesa ya mfukoni ya Tarimba kwa hiyo wana Yanga wasitetereke na tumeshaanza kufanya usajili," ameongeza Makele.

Jana Tarimba alijiondoa kwenye Kamati Maalum ya Mpito ambayo yeye alikuwa Mwenyekiti sababu kubwa aliyotoa ikiwa ni muingiliano wa majukumu baina ya Kamati yake na nyingine pia kukosa ushirikiano kutoka kwa uongozi wa Yanga
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’