Winga machachari wa Mbeya City Mrisho Ngassa 'Uncle' yuko kwenye mazungumzo na uongozi wa Yanga na huenda akasaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Yanga.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya usajili ametuambia kwa kifupi : "Ndio 'Uncle' tunaweza kuwa naye"
Hatma yake itawekwa hadharani mapema kabla dirisha la usajili halijafungwa saa 5.59 usiku.
Ngassa yuko jijini Dar es salaam tangu juzi baada ya kupata mwaliko kutoka kwa viongozi wa Yanga na hata jana alikuwepo pale kwenye uwanja wa Taifa kushuhudia mpambano wa kirafiki kati ya Yanga dhidi ya SIngida United.
Ngassa ilikuwa pengine awe mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Yanga mwezi Juni lakini utaratibu wa kutaka kumsajili uligubikwa na sintofahamu hivyo dili hiyo kukwama.
Alikuwa miongoni mwa wachezaji walio-orodheshwa kuitumikia Yanga kwenye michuano ya SportPesa mapema mwezi Juni.
Aidha, kuondoka kwa Simon Msuva kumetoa nafasi kwa 'Uncle' kuweza kurejea Yanga, mahali ambapo ni nyumbani kwake.
Ngassa alin'gara hapa na si vibaya tukimkaribisha kwa mara nyingine.
Uzoefu wake utaisaidia Yanga ambayo sasa imesheheni vijana wengi.

ADVERTISE HERE