Sauko amshukia Sanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Jul 2018
Sauko amshukia Sanga
Katibu Mipango wa zamani wa Yanga Abdul Sauko amemshukia Kaimu Mwenyekiti wa timu hiyo Clement Sanga akimtaka aache kuingiza Yanga kwenye mgogoro.

Sanga anadaiwa kuwa sababu ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mpito, Abbas Tarimba baada ya 'kuiponda' kamati yake kwenye mkutano wa wenyeviti wa matawi ya klabu ya Yanga juzi.

Katika Mkutano huo pia Sanga aliwaeleza wenyeviti wa Matawi ya Yanga kuwa wameivunja Kamati hiyo baada ya kuona haina msaada kwa Yanga

Sauko amesema Sanga hayupo Yanga kutetea maslahi ya timu, analinda maslahi yake hasa Uwenyekiti wa Bodi ya Ligi.

Aidha Sauko ameunga mkono kujiuzulu kwa Tarimba akieleza Kamati yake ambayo iliundwa na Wanachama siku ya Mkutano Mkuu imebadilishwa majukumu na uongozi wa Sanga kwa maslahi yake.

"Tunafahamu Sanga ni Mwenyekiti wa Bodi ya ligi kupitia Yanga. Anajua akiondolewa Yanga leo atapoteza sifa ya kuendelea kuongoza bodi hiyo," Sauko ameiambia EFM.

"Anachokifanya sasa ni kuwahadaa wanachama wa klabu ya Yanga ili aendelee kulinda maslahi yake."

"Kamati ya Tarimba iliundwa ili kuivusha Yanga kwenye kipindi hiki kigumu. Siku ya Mkutano Mkuu Wanachama wa Yanga walishangilia kuundwa kwa Kamati hiyo kwa kuwa waliamini itakuwa mkombozi."

Bado kumekuwa na sintofahamu juu ya hatma ya Kamati hiyo ya mpito baada ya kujiuzulu kwa Mwenyekiti jana huku baadhi ya wajumbe wake wakidaiwa kujiweka kando.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’