Tarimba aachia ngazi Kamati ya Mpito

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Jul 2018
Tarimba aachia ngazi Kamati ya Mpito
Mwenyekiti wa Kamati ya Mpito Abbas Tarimba ametangaza kujiuzulu nafasi yake kwa kile alichoeleza kuingiliana kwa majukumu baina ya Kamati yake na Kamati ya usajili.

Kamati ya Mpito iliundwa kuivusha Yanga kipindi hiki cha usajili na Bodi ya Wadhamini siku ya Mkutano Mkuu wa Wanachama wa timu hiyo, Juni 10, 2018.

Kazi kubwa waliyopewa ikiwa kukusanya fedha zitakazowezesha kufanya usajili wa wachezaji wapya pamoja na kuhuisha mikataba ya wachezaji iliyokuwa imemalizika.

Hata hivyo Tarimba amesema Kamati yake ni kama imebadilishiwa majukumu sasa, tofauti na awali, wao wametakiwa kukusanya fedha huku jukumu la kufanya usajili wakitakiwa waliache kwa Kamati ya Usajili inayoongozwa na Hussein Nyika.

"Kumekuwepo muingiliano wa majukumu baina ya kamati yangu na kamati ya usajili. Sasa tunaambiwa Kamati yetu ni ya kukusanya fedha tu. Mi nilidhani tulipewa jukumu la ujumla la kuivusha Yanga," amesema Tarimba.

Tangu kuundwa kwa Kamati ya Mpito, kumekuwa na ushirikiano hafifu baina ya Kamati hiyo na Kamati ya usajili.

Aidha Tarimba amewataka viongozi wa Yanga wawe wakweli wasiwapotoshe wapenzi na wanachama wa klabu hiyo kongwe zaidi nchini.

"Nawaambia viongozi wa Yanga waachane na mimi, mimi sina muda wa kuonana na Sanga waachane na mimi, yeye kwanza kamati kaisha ivunja na hata kama wasingevunja mimi nisingeweza kufanya kazi nao"

"Nawaomba viongozi wa Yanga waache usanii, waache ngonjera za uongo, Yanga ni taasisi kubwa"

"Tukipata viongozi wa aina hii ya Yanga hawatafika kokote sijawahi kuona viongozi wa aina hii Yanga

"Kuna mambo mengine siwezi kuongea hapa mimi napenda umoja ndani Yanga kwa sasa sitaki kujihusisha na Yanga"

"Wana Yanga mnadanganywa yaani wanayanga mnadanganywa mchana kweupe, Yanga tuna tamaduni zetu sio hizi, viongozi ni waongo ,nawaomba watulize akili zao wasaidie timu.

"wengine ni wakubwa wanaongoza mpaka bodi ya ligi ,sasa watumie ukubwa huo kuipeleka Yanga mbele waache uongo uongo"
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’