Wazambia wamnyemelea Kessy

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Jul 2018
Wazambia wamnyemelea Kessy
Kuna taarifa kuwa beki wa kulia wa Yanga Hassani Ramadhani Kessy ameingia kwenye rada za klabu ya Nkana Red Devils inayoshiriki ligi kuu ya Zambia.

Kessy alin'gara kwenye kikosi cha Yanga msimu uliopita na alichaguliwa miongoni mwa wachezaji 11 waliotinga katika kikosi bora cha VPL 2017/18.

Kessy ni miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao imemalizika na sasa wako kwenye mazungumzo ya kuongeza mikataba mipya katika klabu ya Yanga.

Wazambia hao wanadaiwa kumpa ofa ya dola 35,000 (zaidi ya Mil 70).

Hivi karibuni Mwenyekiti wa Kamati ya ysajili ya Yanga Hussein Nyika alisema hakuna mchezaji ambaye yuko kwenye mipango ya Yanga ataondoka.

Yanga tayari imefanikiwa kuwabakisha nyota wake waandamizi isipokuwa Obrey Chirwa ambaye ametimkia Misri klabu ya Ismailia.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’