Yanga inajiandaa na mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Gor Mahia utakaopigwa siku 10 zijazo jijini Nairobi, Kenya.
Hata hivyo timu hiyo imekuwa ikijifua pasi na kuwa na vifaa vya mazoezi vinavyotolewa na CAF kwa timu zote zinazoshiriki michuano hiyo.
Uongozi wa Yanga umeshangazwa na ukimya wa TFF ambayo ilipaswa kufuatia vifaa hivyo kwani ni wajibu wao.
Akizungumza mapema leo, Katibu wa Matawi ya Yanga nchini, Boaz Ikupilika amesema timu nyingine zote zinazoshiriki michuano hiyo zimekabidhiwa vifaa hivyo na mashirikisho yao isipokuwa Yanga.
Katika hatua nyingine, Ikupilika ameitaka TFF iilipe Yanga fedha zake za mshindi wa tatu za msimu uliopita.
Amesema TFF imezuia malipo hayo halali ya Yanga.

ADVERTISE HERE