Heritier Makambo, Deus Kaseke na Mrisho Ngassa ndio wachezaji watatu walioongezwa kwenye kikosi cha Yanga kinachoshiriki michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Wachezaji hao tayari wamesajiliwa na watakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachoivaa Gor Mahia Julai 18 jijini Nairobi Kenya.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga Hussein Nyika amesema wamewaongeza wachezaji hao baada ya kuridhishwa na uwezo wao.
Aidha Nyika amesema uzoefu wao utaweza kukiimarisha kikosi cha Yanga ambacho kimedhamiria kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho.
Yanga inatarajiwa kuondoka wakati wowote kwenda mkoani Arusha kuweka kambi kuendelea na maandalizi ya mchezo ujao dhidi ya Gor Mahia

ADVERTISE HERE