Mjumbe wa Kamati ya Kuisaidia Yanga, Abdallah Bin Kleb amejiweka pembeni kwenye kamati hiyo kutokana na sababu za kiafya na kubanwa na majukumu.
Katika barua yake iliyoandikwa Juni 26 mwaka huu, Bin Kleb amedai kuwa kwa sasa muda mwingi amekuwa akiutumia kwa ajili ya matibabu jambo litakalomfanya asipate muda wa kutosha kutimiza majukumu hayo.
Bin Kleb amedai pia kuwa mbali na matatizo ya kiafya, majukumu ya kikazi ambayo hakutaka kuyaainisha yatamfanya ashindwe kumudu kuitumikia kamati hiyo maalum.
Hata hivyo Bin Kleb amedai kuwa ataendelea kuisaidia Yanga muda wowote pindi atakapohitajika kufanya hivyo.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE