Wakati zikiwa zimebaki wiki mbili tu kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Gor Mahia utakaopigwa Julai 19 Nairobi Kenya, Yanga imekamilisha usajili wa wachezaji watatu ambao majina yao yametumwa shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) ili waweze kutumika kwenye michuano hiyo.
Leo ndio ilikuwa siku ya mwisho ya kuwasilishwa kwa usajili wa nyongeza kwa timu ambazo awali zilituma majina pungufu ya 30.
Yanga ilikuwa na nafasi tatu ambazo Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya timu hiyo Hussein Nyika amethibitisha kuwa tayari wamezijaza kwa kutuma majina ya wachezaji hao CAF.
Hata hivyo Nyika aligoma kuweza wazi majina ya wachezaji hao akieleza kazi hiyo itafanywa na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa.

ADVERTISE HERE