Rasta Jaffar Mohammed ni miongoni wa wachezaji waliomvutia kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera na inaelezwa kiraka huyo aliyetokea Majimaji yuko mbioni kusajiliwa.
Uwezo wake wa kucheza nafasi zote za pembeni pamoja na kiungo umemfanya awe mchezaji wa tofauti ambaye Zahera anaamini ataweza kuisaidia Yanga msimu ujao.
Jaffar ni mchezaji huru baada ya mkataba wake wa kuitumikia Majimaji kumalizika.
Mbali na Jaffar wachezaji wengine ambao wamewashiwa taa ya kijani na benchi la ufundi ni pamoja na Mrisho Ngassa, Heritier Makambo na nyota Mnigeria aliyetoka Serbia Emeka Emerun ambaye Zahera amemuona siku moja tu na kuridhika kwamba ni kifaa.
Jana Meneja wa Yanga Hafidh Saleh alisema timu hiyo iko mbioni kumaliza zoezi la majaribio kazi kubwa waliyonayo sasa ikiwa ni kuchuja majina sita ya nyota wa kigeni waliyobaki nayo.
Yanga ina nafasi tatu za nyota wa kigeni zilizowazi baada ya kuondoka kwa Obrey Chirwa, Fiston Kayembe na Donald Ngoma.

ADVERTISE HERE