Yanga ya Zahera itakuwa moto wa kuotea mbali

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Jul 2018
Yanga ya Zahera itakuwa moto wa kuotea mbali
Wakati zikiwa zimebaki wiki tatu kabla ya dirisha kubwa la usajili kufungwa Julai 26, Yanga bado haijaweka hadharani kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao.

Mchakato wa usajili umekuwa ukifanyika kwa usiri mkubwa huku kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera akisisitiza ni lazima awafanyie majaribio wachezaji wanaotaka kutua Jangwani.

Utaratibu huu umezua sintofahamu miongoni mwa mashabiki wa Yanga lakini umewapoteza 'maboya' wapinzani wao ambao wanaamini timu hiyo inasuasua kwenye usajili kwa kuwa haina fedha.

Lakini kwa mchakato unavyoelekea Jangwani, hakuna shaka kikosi cha mabingwa hao wa Kihistoria Tanzania Bara kitakuwa imara msimu ujao kama ilivyo kawaida yake.

Uamuzi uliochukuliwa na Bodi ya Wadhamini ya timu hiyo kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama Juni 10 wa kuunda Kamati Maalumu ya mpito inayoongozwa na Rais wa zamani wa Yanga, Abbas Tarimba, umekuwa wa manufaa.

Mbali na majukumu mengine, Kamati hiyo ilipewa kazi ya kusaka pesa ili kuiwezesha Yanga kufanya usajili wa maana.

Baada ya kutambulishwa, Tarimba aliwaambia Wana Yanga watulie kwa kuwa timu hiyo itafanya usajili makini utakaorejesha makali yake.

Ndio maana leo Yanga imeweza kuleta zaidi ya wachezaji 14 wa kigeni kufanya majaribio katika klabu hiyo.

Lakini ni juzi tu Yanga imemleta mshambuliaji aliyekuwa anacheza soka Barani Ulaya, Mnigeria Emeka Emerun ambaye anakaribia kumalizana na uongozi wa timu hiyo.

Utaratibu unaotumiwa na Yanga kusajili wakati huu unadhihirisha dhamira ya viongozi wa timu hiyo kutengeneza kikosi imara.

Zahera alipendekeza utaratibu huo na tayari umeonyesha kuwa na manufaa kwani umeondoa ubabaishaji katika usajili.

Kupitia utaratibu huo Yanga imejihakikishia kusajili wachezaji 'wa kazi'.

Kwa wale wanaodhani Yanga imekwisha waweke akiba ya maneno, muda utazungumza.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
39m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’