Uongozi wa Yanga umethibitisha kuondoka kwa mshambuliaji wake Obrey Chirwa aliyesajiliwa na klabu ya Ismailia ya Misri.
Jana Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika alisema timu hiyo haikuweza kumzuia mshambuliaji huyo asiondoke baada ya mkataba wake kumalizika.
Ukiachana na Chirwa, Yanga imefanikiwa kuwazuia wachezaji wake wengine ambao mikataba yao imemalizika wasiondoke.
Nyika amesisitiza kuwa hakuna mchezaji ambaye ataondoka kama Yanga bado inamuhitaji.
Idadi kubwa ya wachezaji walioitumikia Yanga msimu uliopita huenda wakaendelea kubaki Jangwani huku uongozi wa timu hiyo ukifikiria kuwatoa kwa mkopo baadhi ya wachezaji wake chipukizi.

ADVERTISE HERE