Ujerumani, Argentina, Ureno na Hispania zimesharejea nyumbani baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya kombe la dunia inayoendelea nchini Urusi.
Leo vigogo wengine Brazil na Ubelgiji wanashuka kwenye viwanja tofauti kusaka tiketi ya kutinga robo fainali ya michuano hiyo.
Mchezo wa mapema saa 11 utakuwa kati ya Brazil dhidi ya Mexico na kufuatiwa na mchezo kati ya Ubelgiji dhidi ya Japani saa tatu usiku.
Kwa takwimu za kwenye karatasi, Brazil inapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi dhidi ya Mexico na hali iko hivyo kwa Ubelgiji dhidi ya Japani.
Lakini tayari baadhi ya michezo ya hatua ya 16 bora imetoa matokeo tofauti na matarajio ya wengi.
Jana Hispania ilitolewa na Urusi huku Croatia ikiiondosha Denmark zote kupitia ushindi wa changamoto ya mikwaju ya penati.
Lakini kama Brazil na Ubelgiji zilizosheheni nyota 'kibao' zitashinda michezo yao leo basi zitakutana kwenye mchezo wa robo fainali, mchezo ambao wengi wanautabiri utakuwa fainali kabla ya fainali!

ADVERTISE HERE