Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera sio mtu wa masihara. Kwa kipindi kifupi alichokaa Yanga ameweza kufanya mabadiliko makubwa huku uongozi ukimuunga mkono.
Zahera amesimamia kikamilifu zoezi la usajili linaloendelea wakati huu baada ya kuagiza wachezaji wote wanaotaka kusajiliwa na Yanga wafanyiwe majaribio bila ya kujali majina yao au timu wanazotoka.
Hata hivyo tangu mkataba wa Shedrack Nsajigwa umalizike, bado Yanga haijatangaza kocha msaidizi wa timu hiyo. Zahera amekuwa akifanya kazi mwenyewe.
Jana Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten alisema timu hiyo bado inaendelea na mchakato wa kusaka kocha msaidizi.
Jina la kocha Mkuu wa Kagera Sugar Mecky Mexime limekuwa likitajwa sana ikielezwa kuwa Yanga imempa ofa ya kumtaka atue Jangwani arithi mikoba ya Nsajigwa.
Lakini pia kocha wa zamani wa KMC, Fredy Felix Minziro anaweza kufaa pia.
Minziro ni kocha asiyetaka masihara, anashabihiana kabisa na Zahera.
Minziro amedhihirisha ubora wake kwa kuzipandisha daraja timu kadhaa kutoka ligi daraja la kwanza.
Msimu uliomalizika, Minziro aliipandisha daraja KMC lakini timu hiyo inayomilikiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imemuondoa kwenye nafasi yake na kumteua Etienne Ndayiragije aliyekuwa kocha wa Mbao FC huku yeye akiahidiwa kupewa cheo kingine.
Ikumbukwe ni Minziro aliyeipandisha daraja Singida United mwaka jana kisha nafasi yake kuchukuliwa na Hans van Pluijm ambaye sasa amekwenda Azam FC.
Licha ya mafanikio aliyozipa Singida United na KMC, inashangaza kuona timu hizo zilimuondoa kwenye nafasi yake.
Minziro anaifahamu vizuri falsafa ya soka la Yanga kwani amekuwa mchezaji wa mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania Bara kwa muda mrefu.
Yanga huenda ikatangaza jina la kocha wake Msaidizi siku itakayotangaza usajili wake wa msimu huu.

ADVERTISE HERE