Mavugo anaweza kufanya maajabu ya Tambwe Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Jul 2018
Mavugo anaweza kufanya maajabu ya Tambwe Yanga
Amissi Tambwe aliachwa na Simba na akatua Yanga akiwa mchezaji huru.

Mabosi wa Yanga waliona Tambwe alikuwa na kitu ambacho Simba hawakukiona ndio maana wakaamua kumsajili saa chache kabla ya dirisha la usajili kufungwa mwaka 2015.

Tambwe akaisaidia Yanga kutwaa ubingwa wa VPL katika misimu yake miwili ya kwanza huku akiibuka kuwa mfungaji bora kwa ujumla katika kipindi cha miaka mitano.

Mkataba wa mshambuliaji Laudit Mavugo na Simba umemalizika na ni dhahiri timu hiyo imeachana nae baada ya kusajili washambuliaji wanne.

Lakini Mavugo alitua Simba misimu miwili iliyopita akiwa mmoja wa wachezaji bora kabisa.

Kwa misimu miwili mfululizo aliibuka kuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Burundi kabla ya Simba kumsajili na kumfanya kuwa mchezaji ghali zaidi kwenye kikosi chao.

Ukimuangalia Mavugo, utakubaliana nami mshambuliaji huyo bado anayo makali. Msimu wake wa kwanza akiwa Simba alifunga mabao nane wakati msimu uliomalizika alifunga mabao matano.

Ukweli ni kwamba hakupata nafasi ya kutosha kuonyesha uwezo wake na pengine hii ilitokana na presha ya mashabiki waliokuwa 'wamemchoka'.

Mara nyingi misimu ya kwanza huwa ni migumu kwa wachezaji wa kigeni hasa wanaotoka ukanda wa Afrika Mashariki. Lakini wakivumiliwa huwa wanakuja kufanya vizuri baadae.

Inaelezwa Yanga tayari imewasilisha ofa ya kutaka kumsajili Mavugo.

Kwa sasa mshambuliaji huyo yuko kwao nchini Burundi na mwenyewe amekiri kuwa katika mazungumzo ya uongozi wa Yanga baada ya kukataa mkataba wa mwaka mmoja aliokuwa amepewa na Simba.

KMC na Singida United nazo zinamuwania mshambuliaji huyo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
12h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
15h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
16h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
17h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’