Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameutaka uongozi wa timu hiyo kuboreshwa timu ya vijana kwa manufaa ya baadae.
Zahera amesema moja ya faida ya kuwa na timu nzuri ya vijana ni wakati huu wa usajili ambapo wachezaji wanaweza kuuzwa, achilia mbali wale ambao wanaweza kupandishwa kwenye timu ya wakubwa hivyo kupunguza gharama za usajili.
Zahera ameahidi kusimamia mchakato wa maboresho ya Yanga B ili kuifanya timu hiyo iwe ya ushindani.
Hivi karibuni Yanga B ilishiriki michuano ya kombe la Uhai mkoani Dodoma na kuondoshwa katika hatua ya makundi baada ya kutoka sare michezo yake yote mitatu.
Tayari uongozi wa Yanga umekuja na mchakato wa kusaka vipaji ambapo hivi karibuni uliwatumia wachezaji wakongwe waliopita katika klabu hiyo miaka ya nyuma kuendesha zoezi la kusaka vipaji

ADVERTISE HERE