Uruguay imeungana na Ufaransa kuwa timu za kwanza kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la dunia baada ya kuilaza Ureno mabao 2-1.
Mabao yote mawili ya Uruguay yalifungwa kwa ustadi mkubwa na Edison Cavan huku bao pekee la Ureno likiwekwa kambani na mkongwe Pepe.
Licha ya jitihada za kusaka bao la kusawazisha, Ureno iliyokuwa ikiongozwa na mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo ilishindwa kufua dafu mbele ya safu imara ya ulinzi ya Uruguay iliyokuwa chini ya mkongwe Godin.
Michuano hiyo sasa itawakosa wanasoka bora zaidi duniani, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo baada ya Argentina na Ufaransa zote kutolewa.
Uruguay itachuana na Ufaransa kwenye mchezo wa robo fainali.
Kesho Jumapili wenyeji Urusi watakuwa na wakati mgumu watakapoikabili Hispania saa 11 jioni katika mchezo mwingine wa kusaka tiketi ya kutinga robo fainali.
Mchezo mwingine utapigwa saa tatu usiku kati ya Croatia dhidi ya Denmark.

ADVERTISE HERE