Serikali kupitia Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe iliutaka uongozi wa Yanga kuhakikisha unajaza nafasi zilizowazi katika muda wa siku si zaidi ya 60.
Miongoni mwa nafasi zilizowazi ni Mwenyekiti wa klabu hiyo na Wajumbe wawili wa Kamati ya Utendaji.
Uchaguzi wa Mwenyekiti haukufanyika siku ya Mkutano Mkuu Juni 10 baada ya wanachama wa Yanga kukataa ombi la kujiuzulu nafasi yake Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuph Manji kupitia barua aliyoiandika mwezi May 2017.
Hata hivyo kumekuwa na ukimya juu ya kurejea kwa Manji ingawa Kaimu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga amethibitisha kuwa tayari walishamuandikia Manji barua kumjulisha uamuzi wa Mkutano Mkuu.
Yanga italazimika kufanya uchaguzi kabla ya August 10 kukidhi masharti ya Serikali kama Manji atashindwa kurejea katika nafasi yake.
Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema 'michakato ya ndani' ndio imewafanya washindwe kujaza nafasi hizo mpaka sasa lakini watalazimika kutii agizo la Serikali kama michakato hiyo itakwama.

ADVERTISE HERE