Mashabiki Yanga waaswa wawe wavumilivu

Suleiman Sudi By Suleiman Sudi
β€’
29 Jun 2018
Mashabiki Yanga waaswa wawe wavumilivu
Yanga bado haijatangaza wachezaji iliyowasajili kwa ajili ya msimu ujao. Ni jambo la kushangaza kuona baadhi ya mashabiki wa timu hiyo wamekuwa na hofu kubwa wakati hata wachezaji waliosajiliwa hawajawafahamu.

Mara kadhaa viongozi wa Yanga wamewataka mashabiki wao wawe watulivu kwani wanaendelea na usajili wakiahidi kutangaza baada ya zoezi hilo kukamilika.

Lazima ifike wakati WanaYanga wakubaliane na hali halisi. Usajili unaofanywa na timu hiyo ni kwa mujibu wa mahitaji na bajeti yao.

Usajili wao hauwezi kufanana na timu nyingine yoyote. Na ndio maana hata utaratibu wanaotumia Yanga ni tofauti na ule unaotumiwa na timu nyingine.

Mashabiki wa Yanga wamekuwa wakipandwa na presha wanapoona wapinzani wao wanasajili wachezaji wapya kila kukicha lakini wanasahau mazingira wanayopitia.

Kwa wakati huu hakuna muujiza utatokea Jangwani. Na ndio maana timu hiyo iliunda Kamati ya mpito iliyopewa kazi ya kusaka pesa ili kuweza kuivusha Yanga katika kipindi hiki cha usajili.

Kamati hiyo inafanya kazi yake na wanapaswa kupongezwa kwani pengine hali ingekuwa mbaya zaidi kama sio uwepo wao.

Huu ni wakati wa kujipanga kwa Yanga. Mazingira ya kifedha ya mabingwa hao wa kihistoria Tanzania Bara hayalingani na mazingira ya watani zao.

Hata Simba iliwahi kupita nyakati kama hizi ambazo Yanga inapita leo. Lakini jambo jema ni kwamba nyakati hizi huwa ni za muda mfupi tu kama viongozi watachukua hatua haraka.

Vilabu vya Yanga na Simba vina 'utajiri' mkubwa wa mashabiki. Vilabu hivi kuingia kwenye dimbwi la umasikini vinajitakia vyenyewe.

Yanga itarejesha 'ubabe' wake kama itaanza kutumia mfumo mpya wa uendeshaji kama ulivyoridhiwa na wanachama wake kupitia Mkutano Mkuu uliofanyika Juni 10 mwaka huu.

Yanga ilikuwa timu ya kwanza kubadili Katiba yake kuruhusu Mabadiliko lakini inashangaza kuona inasuasua kuanza matumizi ya mfumo huo.

Zile zama za kumtegemea mtu mmoja zimewaponza Yanga na hakika hawapaswi kufanya makosa ya kurejea kulekule.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
17h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
22h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
2d ago
READ MORE β†’