Yanga inaendelea kujifua Kurasini

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Jun 2018
Yanga inaendelea kujifua Kurasini
Kikosi cha Yanga kimeendelea kujifua katika uwanja wa chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam chini ya kocha wake Mkuu Mwinyi Zahera.

Yanga ilianza mazoezi na wachezaji nane iliyokuwa nao msimu uliopita lakini idadi imekuwa ikiongezeka siku hadi siku.

Katika mazoezi hayo pia kumekuwa na idadi kubwa ya wachezaji wapya wanaofika kujaribiwa ikiwa ni maagizo ya kocha Mkuu wa timu hiyo.

Wachezaji wa Kimataifa nao wameendelewa kujaribiwa ili kujiridhisha na viwango vyao kabla ya kuwasajili.

Ifahamike wachezaji wote wanaojaribiwa wametakiwa na Yanga, si kwamba wamejipeleka wenyewe. Wengi wametoka timu zinazoshiriki ligi kuu katika mataifa mbalimbali barani Afrika.

Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Usajili amesema tayari kuna wachezaji wamefuzu majaribio hayo na wanakamilisha kuwasajili.

Moja ya masharti yaliyowekwa na Yanga ni kuwa baada ya mchezaji kufuzu majaribio atafanyiwa vipimo vya afya kubaini utimamu wa afya yake kabla ya kusaini mkataba

Msimu uliomalizika Yanga ilikumbwa na changamoto ya wachezaji waandamizi kuwa majeruhi, imedhamiria kusajili wachezaji wenye afya timamu.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika amesema zoezi la usajili liko mbioni kukamilika na kwa wakati muafaka watatangaza wachezaji waliosajiliwa na wale waliopewa mkono wa kwa heri.

Dirisha la usajili lilifunguliwa Juni 15, 2018 na litafungwa Julai 26 2018.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’