Kiungo mshambuliaji wa Singida United Deus Kaseke yuko mbioni kurejea katika kikosi cha Yanga, imefahamika.
Kaseke alitua Singida United akitokea Yanga baada ya kukamilika kwa msimu wa 2016/17 ambao Yanga ilitwaa taji la VPL kwa msimu wa tatu mfululizo.
Kumekuwa na majadiliano kati ya Yanga na Singida United juu ya mchezaji huyo ambaye bado ana mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia Singida United.
Awali Kaseke alikuwa akihusishwa na kutimkia Afrika ya Kusini.
Mwenyewe amekiri kuwepo kwa mazungumzo hayo baina ya Yanga na Singida United.
Amesema makubaliano yakifikiwa atajiunga na Yanga.
Yanga inataka kumuongeza Kaseke kwenye kikosi chake kinachoshiriki michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika, akiwa miongoni mwa wachezaji watatu watakaosajiliwa wakati huu kwa ajili ya michuano hiyo.

ADVERTISE HERE