Maombi ya Mwenyekiti wa zamani wa Yanga Yusuph Manji ya kuomba apewe dhamana katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili yameshindwa kusikilizwa leo kufuatia Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Isaya Arufani ambaye anasikiliza kesi hiyo kutokuwepo Mahakamani.
Manji alipeleka maombi hayo katika mahakama hiyo kupinga hati iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kuzuia dhamana dhidi yake.
Kutokana na jaji huyo kutokuwepo, ombi hilo limesogezwa mbele na linatarajiwa kusikilizwa Agosti 7, mwaka huu.
Manji na wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe, plate number mbili za magari ya serikali jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Katika kesi hiyo ambayo inaendeshwa na Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Huruma Shaidi, leo asubuhi ilitajwa katika mahakama hiyo na kuahirishwa hadi Agosti 9, mwaka huu kutokana na Manji kutofika mahakamani hapo.
Manji alishindwa kufika mahakamani Kisutu kutokana na kuwa na kesi katika Mahakama Kuu.

ADVERTISE HERE