Yanayojiri Urusi : Senagal kuikabili Colombia, Uingereza na Ubelgiji hapatoshi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Jun 2018
Yanayojiri Urusi : Senagal kuikabili Colombia, Uingereza na Ubelgiji hapatoshi
Senegal wawakilishi pekee wa Afrika waliobaki kwenye michuano ya kombe la dunia wataweza kutinga hatua ya mtoano kama watapata hata sare dhidi ya Colombia leo.

Mchezo huo utapigwa saa 11 jioni sambamba na mchezo wa Japani dhidi ya Poland.

Japani na Senegal zinaongoza kundi H zote zikiwa na alama nne wakati Colombia iliyojikusanyia alama tatu inahitaji kuifunga Senegal ili iweze kutinga hatua ya mtoano.

Uingereza na Ubelgiji zitachuana saa tatu usiku kwenye mchezo mwingine wa kusaka kinara wa kundi G kwa kuwa timu zote tayari zimefuzu.

Nazo Panama na Tunisia zitachuana kusaka heshima kwa kuwa tayari zote zimeshaondoshwa kwenye michuano hiyo.

Jana Brazi iliilaza Serbia mabao 2-0 kwenye mchezo wa usiku na kutinga hatua ya mtoano ikiongoza kundi E baada ya kufikisha alama saba ikifuatiwa na Uswisi iliyolazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Costa Rica.

Brazil itacheza na Mexico kwenye hatua ya 16 bora wakati Uswisi itamenyana na Sweden.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
2h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
20h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’