Ukifuatilia mwenendo wa usajili wa klabu ya Simba utakubaliana nami kuwa timu hiyo imekuwa ikifuata 'kivuli' cha Yanga kwa kusajili wachezaji ambao yawezekana wamekuwa kwenye mazungumzo ya kutaka kusajiliwa na Yanga au wengine wametajwa tu na vyombo vya habari kuwa wanawindwa na Yanga.
Ukiwasikiliza mashabiki wa Simba wao wanafurahia hali hiyo wakidai kuwa 'wanalipa kisasi' kutokana na mateso waliyoyapata miaka ya nyuma kwa Yanga kusajili wachezaji wao.
Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Yanga, Abbas Tarimba wakati akihojiwa kwenye kipindi cha michezo cha EFM ameponda utaratibu huo wa Simba na kudai timu hiyo haina wataalamu wa kusaka wachezaji 'Scouting' ndio maana wanasubiri kusajili wachezaji wanaotajwa Yanga.
Mpaka sasa Simba imesajili washambuliaji wanne wengi wao wakiwa walihusishwa kutakiwa na Yanga iwe kwa kutajwa na vyombo vya habari au kuthibitishwa na viongozi.
Na bado inahusishwa kutaka kuwasajili wengine wanaotajwa kuwaniwa na Yanga.
Ninachofahamu, hakuna timu itafanya usajili wa kukomoa timu nyingine kwa kuwa tu ina jeuri ya fedha halafu ikafanikiwa.
Timu makini husajili kulingana na mahitaji yake ambayo yanakwenda sambamba na mapendekezo ya kocha.
Unaposajili kwa kukomoa maana yake utasajili bila kujali mahitaji yako kwani utasajili wachezaji ambao wengine tayari unao kwa kuwa tu wanatakiwa na mpinzani wako.
Sikumbuki kama Yanga imewahi kufanya usajili wa kuikomoa Simba. Idadi kubwa ya wachezaji waliotamba nchini tangu zamani wamekuwa wakiletwa na Yanga kufuatana na mahitaji ya timu hiyo.
Yanga imeendelea na utaratibu huo wa kuibua wachezaji wakali kutoka mataifa ya mbali ambao kabla walikuwa hawajulikani.
Wachezaji kama Kamusoko, Donald Ngoma, Obrey Chirwa, Tshishimbi na wengine wengi waliletwa baada ya kufanyiwa 'scouting' nzuri wakati Yanga ikishiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
Hakuna aliyekuwa akiwafahamu kabla ya kutua Yanga.
Hakuna shaka zoezi la usajili linalofanywa na viongozi wa Yanga litaibuka na wachezaji wakali ambao watawaduwaza wale waliozoea kusajili wachezaji walewale kwa mbwembwe.

ADVERTISE HERE