Uamuzi wa kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera kujiridhisha na uwezo wa baadhi ya wachezaji kabla ya kuidhinisha wasajiliwe ni sahihi sana hasa wakati huu ambao Yanga imekumbwa na changamoto za kiuchumi.
Zahera aligoma kuidhinisha usajili wa mchezaji yeyote ikiwa ni pamoja na wale aliowaleta yeye mwenyewe lengo ikiwa ni kuhakikisha benchi zima la ufundi linajiridhisha na uwezo wao.
Utaratibu huu utaisaidia Yanga kuwa na uhakika na wachezaji inaowasajili lakini ni lazima ifanye haraka kukamilisha zoezi hilo.
Kwani kama litachukua muda mrefu haitashangaza kusikia baadhi ya wachezaji wakitimkia timu nyingine licha ya Yanga kuingia gharama ya kuwaleta nchini.
Zile timu zilizoapa kusajili 'wachezaji wa Yanga' bado zipo na hakika hazitasita kutumia mwanya huo kama zitabaini kuna wachezaji wazuri bado hawajasaini mikataba.
Pia ikumbukwe Yanga ina mchezo dhidi ya Gor Mahia Julai 18. Ni lazima ianze maandalizi mapema kuelekea mchezo huo.
Yanga ikitumia muda mwingi kujaribu wachezaji, itachelewa kufanya maandalizi ya kutosha kuelekea mchezo huo.

ADVERTISE HERE