Yanayojiri Urusi : Argentina yapenya hatua ya mtoano, yailaza Nigeria 2-1

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Jun 2018
Yanayojiri Urusi : Argentina yapenya hatua ya mtoano, yailaza Nigeria 2-1
Argentina imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya kombe la dunia baada ya kuilaza Nigeria mabao 2-1 katika mchezo mkali uliopigwa dimba la St Petersburg Jumanne usiku.

Lionel Messi aliitanguliza Argentina kwa bao safi kwenye dakika ya 14 lakini Nigeria wakarejea mchezoni kwenye kipindi cha pili, dakika ya 51 kwa bao la mkwaju wa penati lililofungwa na Victor Mosses.

Matokeo ya sare yangetosha kuivusha Nigeria lakini beki wa Manchester United Marcos Rojo alifuta ndoto za Waafrika baada ya kuifungia Argentina bao safi kwenye dakika ya 86.

Ushindi huo umeifanya Argentina imalize nafasi ya pili kundi D ikiwa na alama nne nyuma ya Croatia iliyomaliza kileleni na alama tisa baada ya kuichapa Iceland mabao 2-1 kwenye mchezo mwingine uliopigwa sambamba.

Kwenye hatua ya 16 bora Argetina itachuana na Ufaransa iliyomaliza vinara wa kundi C licha ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana na Denmark kwenye mchezo wa mapema.

Croatia itamenyana na Denmark.

Nigeria imeungana na timu nyingine za Afrika, Tunisia, Morocco na Misri kuyaaga mashindano hayo na kuiacha Senagal ambayo itafahamu hatma yake keshokutwa itakapochuana na Colombia

Kesho Jumatano kutakuwa na michezi minne ya kundi E na F ambapo saa 11 jioni Mexico itachuana na Sweden wakati huohuo Ujerumani ikichuana na Korea Kusini.

Saa tatu usiku Uswisi itamenyana na Costa Rica na wakati huo huo Brazil ikipepetana na Serbia.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’