Yanga ilivyojipanga kuepuka 'ujanja ujanja' kwenye usajili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Jun 2018
Yanga ilivyojipanga kuepuka 'ujanja ujanja' kwenye usajili
Msimu wa 2017/18 haukuwa mzuri kwa klabu ya Yanga baada ya kukumbwa na changamoto mbalimbali za nje na ndani ya uwanja.

Ukiachilia mbali changamoto za kiuchumi, Yanga iliteswa na majeruhi ya mda mrefu ya wachezaji wake waandamini waliosajiliwa kwa gharama kubwa.

Donald Ngoma aliyetimkia Azam FC, Amissi Tambwe na Thabani Kamusoko walitarajiwa kuibeba Yanga lakini pengine ndio wachezaji waliokuwa na mchango mdogo zaidi kutokana na majeraha yaliyowaweka nje kwa karibu msimu mzima.

Na hii ndio moja ya sababu iliyoifanya Yanga ije kivingine msimu huu katika kukamilisha michakato yake ya usajili.

Yanga imeamua kufanya usajili wa kisasa ambapo sasa ni lazima wachezaji wafanyiwe vipimo vya afya zao kabla ya kupewa mikataba wasaini.

Lakini pia jambo muhimu zaidi ni uamuzi wa kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera kuwajaribu baadhi ya wachezaji hao kabla ya kuidhinisha wasajiliwe.

Yanga imemuachia majukumu ya usajili kocha wake Mkuu ambapo ni yeye anayetoa mapendekezo ya aina ya wachezaji anaowataka na ndiye anayeamua nani asajiliwe.

Yanga inayoanza mazoezi leo itakuwa na wachezaji kadhaa wa Kimataifa ambao tayari wako nchini na huenda wakasajiliwa kama watamridhisha kocha huo aliyedhamiria kusuka Yanga imara.

Alipowasili Jumamosi kutoka mapumziko nchini Ufaransa, alitua na mshambuliaji mwingine ambaye huenda akaanza kuonekana kwenye mazoezi ya Yanga.

Zahera pia amependekeza mikataba watakayoingia wachezaji na klabu ya Yanga iwe na vipengele vitakavyoruhusu mikataba hiyo kufanyiwa tathmini kila baada ya miezi sita.

Tathmini hiyo ikiwa na lengo la kuwanufaisha zaidi wachezaji wanaofanya vizuri huku ikiwagharimu wachezaji watakaokuwa wameshindwa kufikia matarajio ya klabu.

Utaratibu huu huenda ukainufaisha Yanga kwani hakutakuwa na nafasi kwa wachezaji wa aina ya Ngoma ambao walisajiliwa kwa fedha nyingi na bado wakala mshahara wa bure msimu mzima.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’