Sababu zilizotolewa na uongozi wa Yanga juu ya uamuzi wake wa kuficha michakato yake ya usajili sasa zimedhihirika baada ya Simba kuendelea kusajili wachezaji ambao wamehusishwa na mabingwa hao wa Kihistoria wa Tanzania.
Adam Salamba, Mohammed Rashid, Paschal Wawa na Meddy Kagere wote wamesajiliwa na Simba huku Yanga ikiwa timu ya kwanza kuonesha nia ya kuwasajili.
Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa aliwahi kusema kuwa kuna timu kwa kuwa zina fedha wakati huu, zimedhamiria kukomoa kwa kuvuruga mchakato wa usajili wa Yanga kwa kuwasajili wachezaji wote wanaohusishwa na timu hiyo.
Licha ya kuwahi kufanya mazungumzo na Kagere, Yanga iliachana na mpango wa kumsajili mshambuliaji huyo aliyetaka kulipwa fedha za usajili zinazokadiriwa kuwa zaidi ya Mil 200.

ADVERTISE HERE