Hakuna kukata tamaa, kituo kinachofuata ni Club Africain

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1h ago
Hakuna kukata tamaa, kituo kinachofuata ni Club Africain

Baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya MC Alger katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), hakuna muda wa kulia na kuhuzunika kwani mapambano lazima yaendelee.

Jumamosi ijayo, Desemba 5, Yanga itakuwa na kibarua kingine kizito ugenini nchini Tunisia dhidi ya Club Africain, ukiwa ni mchezo wa pili wa hatua ya makundi.

Hii ni mechi itakayohitaji wachezaji wa Yanga kupambana kwa jasho na damu kuhakikisha wanaondoka Tunisia na matokeo chanya.

Kama ilivyo kwa Yanga, Club Africain nao walipoteza mchezo wao wa kwanza ugenini kwa kufungwa bao 1-0 na Zamalek, hivyo pambano hili lina sura ya fainali kwa pande zote mbili.

Mazingira ya mchezo huu yanakumbusha kile kilichotokea mara ya mwisho timu hizi zilipokutana nchini Tunisia katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) mwaka 2022.

Licha ya mazingira magumu waliyokutana nayo wakati huo, Wananchi waliibuka na ushindi wa bao 1-0 na kufanikiwa kutinga hatua ya makundi, katika msimu ambao walikwenda hadi fainali na kukosa ubingwa kwa kanuni ya bao la ugenini baada ya kufungwa mabao 2-1 nyumbani na USM Alger kabla ya kushinda bao 1-0 ugenini.

Yanga si wageni wa mechi za aina hii. Historia inaonyesha kuwa mara kadhaa Wananchi wamekuwa na uwezo wa kuamka ugenini baada ya kupata matokeo yasiyoridhisha nyumbani.

Kilichotokea dhidi ya MC Alger kinapaswa kuwa somo kwa benchi la ufundi na wachezaji, huku siku chache zilizobaki zikitumika kusahihisha makosa na kujiandaa kwa pambano lijalo.

Kupoteza mchezo wa kwanza hakumaanishi kupoteza nafasi ya kufuzu. Bado kuna mechi tano za kupambania tiketi ya hatua ya robo fainali.

Yanga SC Stories

Kazini kwa Mudathir kulikuwa na kazi
Kazini kwa Mudathir kulikuwa na kazi
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumapili, Novemba 29 2026
Magazeti ya leo Jumapili, Novemba 29 2026
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 0-1 MC Alger, CAFCL MD1
FT : Yanga 0-1 MC Alger, CAFCL MD1
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs MC Alger, CAFCL, MD1
Kikosi : Yanga vs MC Alger, CAFCL, MD1
18h ago
READ MORE β†’
Mayele anaamini huu ni mwaka wa Wananchi CAFCL
Mayele anaamini huu ni mwaka wa Wananchi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Ni leo; Yanga inaanza kubonda na kunyonga CAFCL
Ni leo; Yanga inaanza kubonda na kunyonga CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumamosi, Novemba 28 2026
Magazeti ya leo Jumamosi, Novemba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki awapa ujumbe mashabiki Yanga 'tutapambana'
Aziz Ki awapa ujumbe mashabiki Yanga 'tutapambana'
1d ago
READ MORE β†’
Fadlu aichambua MC Alger, aweka mkakati wa ushindi
Fadlu aichambua MC Alger, aweka mkakati wa ushindi
1d ago
READ MORE β†’
Wananchi wajitokeza kuchangia damu Viwanja vya Maturembeta Zanzibar
Wananchi wajitokeza kuchangia damu Viwanja vya Maturembeta Zanzibar
1d ago
READ MORE β†’