Aziz Ki awapa ujumbe mashabiki Yanga 'tutapambana'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
47m ago
Aziz Ki awapa ujumbe mashabiki Yanga 'tutapambana'

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki, ametoa wito kwa mashabiki wa Wananchi kujitokeza kwa wingi na kuwa nyuma ya timu katika dakika zote 90 za mchezo dhidi ya MC Alger ya Algeria, akisisitiza kuwa wachezaji wako tayari kupambana kuhakikisha wanaanza kampeni yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) kwa ushindi.

Yanga itashuka dimbani kesho Jumamosi, Novemba 28, 2026, kuanzia saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, visiwani Zanzibar, kuvaana na mabingwa hao wa Algeria katika mchezo wa kwanza wa Kundi B.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea pambano hilo, Aziz Ki amesema wamekuwa wakisubiri kwa hamu kuanza mikiki mikiki ya hatua ya makundi, huku akieleza kuwa maandalizi waliyofanya yanawapa imani ya kupata matokeo mazuri.

“Wote tumekuwa tukiusubiri kwa hamu wakati huu. Tumefanya maandalizi ya kutosha na tuko tayari kutoa kila kitu uwanjani ili kuanza kampeni yetu ya mashindano haya kwa ushindi.”

ANATAKA NGUVU YA MASHABIKI DAKIKA 90

Aziz Ki ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha mashabiki umuhimu wa mchango wao katika michezo mikubwa ya kimataifa, hasa nyakati ambazo timu inapokutana na changamoto ndani ya uwanja.

Nyota huyo raia wa Burkina Faso hataki kuona mashabiki wakipunguza hamasa pale mambo yanapokuwa magumu, badala yake anataka waendelee kuwapa nguvu wachezaji ili waweze kupambana hadi filimbi ya mwisho.

“Ninawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi, wajaze uwanja na kuunda mazingira mazuri ya kutupa hamasa ya kupambana hadi mwisho.”

Aziz Ki mesisitiza kuwa nguvu ya mashabiki inahitajika si wakati wa kutafuta bao la kwanza pekee, bali hata baada ya kupata bao hilo ili kuwapa wachezaji msukumo wa kuongeza mabao zaidi.

HAKUNA NAFASI YA KUPOTEZA POINTI NYUMBANI

Sambamba na kauli za Kocha Mkuu wa Yanga, Fadlu Davids, ambaye ameweka wazi mikakati yake ya kushinda michezo yote ya nyumbani, Aziz Ki amesema wachezaji wanatambua umuhimu wa kutumia vizuri fursa ya kuanza mashindano mbele ya mashabiki wao.

“Kuanza mashindano tukiwa nyumbani ni faida kubwa kwetu. Hivyo, tuna wajibu wa kutumia vizuri fursa hiyo kwa kufanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha tunapata ushindi mbele ya mashabiki wetu.”

Ushindi dhidi ya MC Alger utakuwa muhimu kwa Wananchi katika harakati zao za kutinga robo fainali baada ya kushindwa kuvuka hatua ya makundi kwa misimu miwili mfululizo.

Yanga SC Stories

Fadlu aichambua MC Alger, aweka mkakati wa ushindi
Fadlu aichambua MC Alger, aweka mkakati wa ushindi
53m ago
READ MORE β†’
Wananchi wajitokeza kuchangia damu Viwanja vya Maturembeta Zanzibar
Wananchi wajitokeza kuchangia damu Viwanja vya Maturembeta Zanzibar
3h ago
READ MORE β†’
Tuko tayari kuikabili MC Alger - Job
Tuko tayari kuikabili MC Alger - Job
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 27 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yakamilisha maandalizi New Amaan Complex tayari kuikabili MC Alger
Yanga yakamilisha maandalizi New Amaan Complex tayari kuikabili MC Alger
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki aweka ahadi, apania ligi ya mabingwa
Aziz Ki aweka ahadi, apania ligi ya mabingwa
1d ago
READ MORE β†’
CAFCL msimu huu VAR kuanza kutumika hatua ya makundi
CAFCL msimu huu VAR kuanza kutumika hatua ya makundi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga ilivyojifua New Amaan Complex, Zanzibar
Yanga ilivyojifua New Amaan Complex, Zanzibar
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Novemba 26 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Novemba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Tom Ambongile kuziamua Yanga na MC Alger CAFCL
Tom Ambongile kuziamua Yanga na MC Alger CAFCL
1d ago
READ MORE β†’