Yanga yatangaza viingilio mchezo dhidi ya MC Alger, CAFCL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29m ago
Yanga yatangaza viingilio mchezo dhidi ya MC Alger, CAFCL

Klabu ya Yanga imetangaza viingilio vya mchezo wake wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya MC Alger ya Algeria, huku kiingilio cha chini kikiwa shilingi 5,000.

Mtanange huo wa Kundi B utapigwa Jumamosi, Novemba 28, 2026, kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, visiwani Zanzibar, huku Wananchi wakilenga kuanza kampeni yao ya hatua ya makundi kwa ushindi.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe, amesema kikosi hicho tayari kimeanza safari kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya mchezo huo.

HIVI NDIVYO VIINGILIO VILIVYOPANGWA

Kwa mujibu wa Kamwe, viingilio vya mchezo huo vimepangwa kulingana na majukwaa mbalimbali ya uwanja huo kama ifuatavyo:

  • Jukwaa la Saa na Obit – Sh 5,000

  • Jukwaa la Urusi – Sh 10,000

  • Wings (pande zote mbili) – Sh 20,000

  • VIP – Sh 30,000

Kamwe amefafanua kuwa tiketi za VVIP hazitauzwa kutokana na eneo hilo kutengwa kwa ajili ya wageni maalumu watakaohudhuria mchezo huo.

TIKETI KUPATIKANA KUPITIA SIMU

Katika kuhakikisha mashabiki wanapata tiketi kwa urahisi, Yanga imeingia katika ushirikiano na Lipa Finance kupitia mfumo wake wa Lipa Tiketi, ambao utawawezesha mashabiki kununua tiketi kwa kutumia simu janja pamoja na simu za kawaida, maarufu kama kitochi.

Shabiki anayetaka kuhudhuria mchezo huo anaweza kukata tiketi kwa kupiga msimbo 14946*11# na kufuata maelekezo, au kutembelea tovuti ya http://yanga.lipatickets.tz/.

“Ni mfumo rahisi na wa haraka utakaomwezesha kila shabiki kupata tiketi yake kwa urahisi na kujipanga kuja kutuunga mkono katika mchezo huu visiwani Zanzibar,” amesema Kamwe.

Kupitia mfumo huo, kila shabiki atakuwa na uwezo wa kununua hadi tiketi nne, huku wale wanaohitaji tiketi kwa idadi kubwa zaidi wakitarajiwa kupewa utaratibu maalumu na Lipa Finance.

Kwa upande wake, Fahad Habib kutoka Lipa Tiketi amesema mfumo huo unalenga kurahisisha upatikanaji wa tiketi, kusimamia ubora wa huduma pamoja na ukusanyaji wa kodi.

KAMWE ATAKA UWANJA UJAEE

Mbali na kutangaza viingilio, Kamwe ametumia nafasi hiyo kuwahamasisha mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi visiwani Zanzibar ili kukipa nguvu kikosi chao katika mchezo huo muhimu.

Kamwe amesema ushindi wa kwanza dhidi ya MC Alger unapaswa kuanzia kwenye ukataji wa tiketi na kujaza uwanja kabla ya kazi kuhamia kwa wachezaji.

“Tunaposema tunakwenda kuwabonda hawa Waarabu, jambo la kwanza ni kuhakikisha tunawabonda kwa kukata tiketi na kujaza uwanja. Tukishafanya hivyo, basi kazi inayofuata ni kwenda kuwabonda ndani ya dakika 90 za mchezo.”

Yanga SC Stories

Kituo kinachofuata ni MC Alger, Zanzibar
Kituo kinachofuata ni MC Alger, Zanzibar
1h ago
READ MORE β†’
Fadlu aweka mkakati hatua ya makundi CAFCL
Fadlu aweka mkakati hatua ya makundi CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Yanga kuelekea Zanzibar leo, maandalizi ya kuikabili MC Alger
Yanga kuelekea Zanzibar leo, maandalizi ya kuikabili MC Alger
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 24 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 24 2026
5h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili MC Alger yanaendelea Gymkhana
Maandalizi ya kuikabili MC Alger yanaendelea Gymkhana
19h ago
READ MORE β†’
MC Alger wamfuta kazi kocha kuelekea mchezo dhidi ya Yanga
MC Alger wamfuta kazi kocha kuelekea mchezo dhidi ya Yanga
20h ago
READ MORE β†’
Kazimoto amkosha Juma Abdul, ampa somo
Kazimoto amkosha Juma Abdul, ampa somo
20h ago
READ MORE β†’
Wanahabari wajitokeza Yanga Media Day
Wanahabari wajitokeza Yanga Media Day
21h ago
READ MORE β†’
Injinia Hersi atabiriwa makubwa CAF
Injinia Hersi atabiriwa makubwa CAF
1d ago
READ MORE β†’
Yanga vs MC Alger, mechi ya kisasi Jumamosi, CAFCL
Yanga vs MC Alger, mechi ya kisasi Jumamosi, CAFCL
1d ago
READ MORE β†’