Kikosi cha Yanga kimeondoka jijini Dar es salaam kuelekea Zanzibar tayari kwa mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL).
Yanga itaanza kampeni ya michuano hiyo kwa mchezo wa kwanza kundi B dhidi ya MC Alger utakaopigwa Jumamosi, Novemba 28 kwenye uwanja wa New Amaan Complex.
Wananchi wameelekea Zanzibar kukamilisha maandalizi ya mwisho kuelekea mtanange huo ambao Yanga inahitaji ushindi ili kuanza vyema hatua hiyo ya makundi.






