Kikosi cha Yanga leo kimejifua viwanja vya Gymkhana jijini Dar es salaam ikiwa ni maandalizi kuelekea mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL).
Jumamosi, Novemba 28 Yanga itashuka uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar kuikabili MC Alger katika mchezo muhimu wa kundi B.








