Wakati Yanga leo ikitarajiwa kushuka uwanja wa Ushirika Moshi kuikabili Polisi Tanzania, Wananchi huenda wakashuhudia urejeo wa kiungo Mudathir Yahya.
Mudathir yuko tayari kurejea kikosini baada ya kumaliza adhabu ya kadi nyekundu aliyopata kwenye mchezo dhidi ya TRA United.
Alikosa mechi mbili zilizopita dhidi ya Mashujaa Fc na Kagera Sugar.
Urejeo wake pia ni ahueni kwa kocha Fadlu Favids ambaye kwenye mchezo wake wa kwanza atamkosa kiungo tegemeo Maxi Nzengeli anayeuguza majeraha ya goti. Maxi anatarajiwa kukosekana kwa takribani wiki sita.
Aidha nyota wengine waliokuwa majeruhi Duke Abuya na Yao Kouassi nao huenda wakarejea leo baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yanawakabili.