Yanga yarejea Dar

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
4 Aug 2017
Yanga yarejea Dar
Klabu ya Yanga imewasili jijini Dar es salaam tayari kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya SIngida United, mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Taifa Jumamosi, Agosti 05.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Afisa Habari kwa Yanga Dismas Ten kwenye mkutano na waabdishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya Yanga jijini Dar es salaam leo, Ten amesema ni wachezaji wawili pekee ambao hawataweza kucheza mchezo huo wa kirafiki kutokana na kukabiliwa na majeruhi.

Ten amewataja wachezaji hao kuwa Obrey Chirwa na Geofrey Mwashiuya ambao wanatarajiwa kuwa nje kwa takribani siku nne.

Naye Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwassa amelaani kitendo kilichofanywa na kampuni ya Vodacom, wadhamini wa ligi, TFF na Bodi ya ligi kwa kushindwa kutoa mwaliko kwa Yanga kwenye sherehe za makabidhiano ya vifaa vya michezo kuelekea msimu mpya.

Mkwasa akizungumza katika Mkutano na waandishi wa habari leo, amesema tukio hilo lisilo la kiungwana limeidhalilisha klabu ya Yanga.

Wakati huo huo Mkwasa amesema zoezi la usajili la klabu ya Yanga limekamilika kwa asilimia 90 na amewatoa hofu mashabiki na wanachama kuwa Yanga itakamilisha taratibu zilizobaki kwa wakati.

Amesema tayari wachezaji waliokamilisha usajili wamesha andikishwa rasmi kwenye mtandao wa FIFA hivyo Yanga haitakuwa miongoni mwa timu ambazo zinaweza kushushwa daraja kwa kushindwa kukamilisha zoezi la usajili kwa wakati.

Amesema Yanga imekamilisha usajili wa wachezaji wote iliyowahitaji na ameelezea kuwa mafanikio hayo yamepatikana baada ya klabu kutumia mfumo wa kusajili kimyakimya.

Mkwasa amesema waliamua kubabili mfumo wa usajili baada ya kubaini baadhi ya timu zilikuwa zinasajili kwa kuangalia kinachofanywa na Yanga.

Amesema anaamini Yanga ndiyo timu pekee iliyosajili wachezaji kwa mpangilio maalumu.

Mkwasa pia amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Taifa kesho Jumamosi wakati Yanga itakaposhuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida United.

Amesema hiyo ni nafasi maalum kwa mashabiki kuishuhudia timu yao na kutoa maoni, mapendekeo na ushauri wao kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii Agosti 23 na msimu mpya wa ligi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
36m ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
15h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
19h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
20h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
20h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’