Jana Colombia ilifufua matumaini ya kutinga hatua ya makundi baada ya kuilaza Poland mabao 3-0 kwenye mchezo wa kombe la Dunia, kundi H.
Mabao ya Yerri Mina, Ramadel Falcao na Juan Quadrado yaliihakikishia Colombia ushindi muhimu ulioweka hai matumaini ya kutinga hatua ya 16 bora kama itaibuka na ushindi kwenye mchezo wake wa mwisho dhidi ya Senegal.
Senegal ililazimishwa sare ya mabao 2-2 na Japan kwenye mchezo ambao ilitangulia kufunga mara mbili lakini ikashindwa kulinda ushindi wake.
Sasa itakuwa na wakati mgumu kuwania nafasi ya kutinga hatua ya 16 bora na Colombia inayoonekana kuimarisha kiwango chake baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Japan.
Sare itatosha kuipeleka Senagal hatua ya 16 bora.
Poland imeyaaga rasmi mashindano hayo baada ya kipigo kutoka kwa Colombia.
Mapema jana Uingereza ilitinga hatua ya mtoano kibabe baada ya kuilaza Panama mabao 6-1.
Harry Kane amewapiku Cristiano Ronaldo na Romelu Lukaku katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu baada ya kufunga hat-trik iliyomfanya afikishe mabao matano.
Leo michezo ya kukamilisha mzunguuko wa kwanza inaanza kupigwa katika wakati mmoja ambapo kundi A na B timu zote zitashuka dimbani.
Saa 11 jioni Saudi Arabia itachuana na Misri na wakati huo huo Uruguay itachuana na Urusi.
Saa tatu siku Irani itachuana na Ureno na huku Hispania ikichuana na Morocco.

ADVERTISE HERE