Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imeondoka na alama moja mbele ya Nigeria baada ya matokeo ya suluhu ya bila kufungana katika mchezo uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar.
Habari njema kwa mashabiki wa Yanga ni kumshuhudia beki Ibrahim Bacca akicheza kwa dakika zote 90 eneo la beki wa kati sambamba na nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto.
Bacca alipata majeraha kwenye mchezo uliopita na kuibua hofu ya kukosa mchezo wa leo.
Hata hivyo beki huyo tegemeo amehimili dakika zote 90 za mchezo huo ambao ulishuhudia Stars ikikusanya alama ya pili.
Aidha mshambuliaji wa Yanga Seleman Mwalimu nae alipata nafasi ya kucheza mchezo huo akiingia kipindi cha pili.
Nyota hao wamekamilisha majukumu yao ya timu za Taifa na sasa wanatarajiwa kurejea kwenye majukumu ya klabu.
Mapema kiungo mshambuliaji Albert Kangwanda nae alikuwa sehemu ya kikosi cha Zambia kilichotoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Burundi ugenini.
Mlinda Djigui Diarra nae yuko kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Mali ambacho kinakamilisha mchezo wa mzunguuko wa nne dhidi ya Rwanda.