Kangwanda, Bacca washusha presha Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4d ago
Kangwanda, Bacca washusha presha Yanga

Daktari wa Yanga Dk Moses Etetu amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuhusu hali za wachezaji Ibrahim Bacca na Albert Kangwanda waliopata majeraha wakati wanazitumikia timu za Taifa.

Yanga imekumbwa na mfululizo wa majeruhi kwa mastaa wake jambo lililopelekea hofu kwa mashabiki katika kipindi hiki muhimu cha msimu.

Akizungumza juzi baada ya mchezo wa kirafki dhidi ya KVZ ambao Yanga ilishinda mabao 3-1, Etutu alisema nyota hao walipata majeraha ya kawaida.

“Kangwanda alipata majeraha kwenye nyama, lakini tumejaribu kuwasiliana naye na tunaona mambo yanaenda vizuri. Ni ‘cramp’ tu, msuli ulichoka akatengeneza tunasema ‘muscle fatigue’.

“Sasa hivi yuko sawa na tunategemea hatakuwa shida nyingine. Tutakuwa naye baada ya hii ratiba ya FIFA na atarejea kwenye timu kama kawaida bila shida yoyote, labda itokee tena shida nyingine kwenye mechi ijayo,” alisema Etutu.

Kwa upande wa Bacca, Dokta Etutu alikiri kuwa beki huyo amepata maumivu kwenye kifundo cha mguu (ankle), lakini akawatoa hofu Wananchi kuwa yupo chini ya uangalizi maalum.

“Bacca amepata maumivu kwenye ‘ankle’ na tuna imani na madaktari wa timu ya taifa wataendelea na matibabu kuona anarejea katika hali nzuri na ya uimara. Atakaporejea kwenye timu tutamfanyia tathmini upya na kuona kiwango cha maumivu aliyonayo ni kiasi gani, kisha tutaendelea na matibabu pale ambapo jopo la madaktari wa timu ya taifa wamekomea,” aliongeza Etutu

Mpaka sasa Yanga inawakosa Mohamed Mussa, Hussein Masalanga na Maxi Nzengeli ambao ni majeruhi huku Duke Abuya na Yao Kouassi wakirejea taratibu

Yanga SC Stories

Goals : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL (FT)
Goals : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
FT : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL
FT : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL
11h ago
READ MORE β†’
Kikosi : JKT Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20
Kikosi : JKT Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20
14h ago
READ MORE β†’
Mudathir amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Mudathir amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Dladla awaaga Wananchi
Dladla awaaga Wananchi
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Polisi Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20
Matchday; Polisi Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yawasili Moshi tayari kuikabili Polisi Tanzania
Yanga yawasili Moshi tayari kuikabili Polisi Tanzania
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yakamilisha maandalizi tayari kuifuata Polisi Tanzania
Yanga yakamilisha maandalizi tayari kuifuata Polisi Tanzania
1d ago
READ MORE β†’
Dikgacoi atamba Yanga ipo tayari kuivaa Polisi Tanzania
Dikgacoi atamba Yanga ipo tayari kuivaa Polisi Tanzania
1d ago
READ MORE β†’