Kikosi cha Yanga leo Jumatatu kinatarajiwa kuhitimisha kambi ya siku 10 visiwani Zanzibar wakitarajiwa kurejea jijini Dar es salaam siku ya Jumanne.
Yanga inakabiliwa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa Ijumaa, Novemba 20 kwenye uwanja wa Ushirika, Moshi.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema timu itarejea Dar es salaam kabla ya safari ya kuelekea mkoani Kilimanjaro.
Yanga ilitua Zanzibar Novemba 08 kwa ajili ya kambi hiyo chini ya kocha Fadlu Davids aliyetua kuchukua mikoba iliyoachwa na Manqoba Mngqithi.
Wakiwa Zanzibar Wananchi walicheza mechi ya kirafiki dhidi ya KVZ juzi na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Kambi hiyo imemsaidia Fadlu kupata utulivue na mwanzo mzuri wa majukumu yake.