Tunajenga falsafa mpya Yanga - Fadlu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Nov 2026
Tunajenga falsafa mpya Yanga - Fadlu

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Fadlu Davids, amefunguka kuhusu falsafa mpya ya soka anayotaka kuijenga ndani ya kikosi hicho, akisisitiza kuwa lengo si kushinda mataji pekee, bali kuifanya Yanga kuwa timu yenye mfumo, utambulisho na aina maalumu ya uchezaji.

Fadlu amesema Yanga imekuwa na mafanikio makubwa kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa misimu mitano mfululizo, lakini sasa umefika wakati wa kujenga msingi imara utakaoiwezesha timu hiyo kuendelea kutawala kwa miaka mingi zaidi.

"Yanga haikosi kushinda, kinachohitajika sasa ni mfumo na philosophy. Tumeshinda ligi kwa miaka mitano mfululizo, lakini tunataka kujenga upya na kudumu. Tunataka kutengeneza playing style yetu, falsafa yetu, kubadilisha mambo polepole na kuongeza wachezaji katika madirisha ya usajili ili Yanga ibaki juu," alisema

Kocha huyo amebainisha kuwa mfumo anaopendelea kuutumia ni 4-2-3-1, ambao unaamini unampa uwiano mzuri kati ya ulinzi na ushambuliaji.

Katika mfumo huo, Yanga itakuwa na mabeki wanne, viungo wawili wa chini wenye jukumu la kulinda safu ya ulinzi na kuzuia mashambulizi ya kushtukiza, kiungo mmoja mshambuliaji mwenye uhuru wa kutengeneza nafasi, pamoja na mawinga wawili watakaokuwa na jukumu la kushambulia na kukata kuelekea katikati.

Fadlu amesema mfumo huo unampa kila mchezaji jukumu maalumu ndani ya uwanja.

"4-2-3-1 ni mfumo unaonipa balance. Mabeki wanne wanalinda, viungo wawili wanazuia counter-attacks, kiungo namba 10 ana uhuru wa kuunda mchezo, mawinga wawili wanashambulia na mshambuliaji mmoja anamalizia. Kila mtu anajua kazi yake."

Mbali na mfumo wa 4-2-3-1, Fadlu anataka Yanga iwe timu inayomiliki mpira, inayowashambulia wapinzani kwa presha kubwa na kurejesha mpira haraka mara inapoupoteza.

Hii ina maana mashabiki wanaweza kutarajia Yanga yenye kasi ya kuzungusha mpira, kucheza kwa nidhamu ya kiufundi na kuwabana wapinzani hata wanapokuwa na mpira.

Amesisitiza kuwa hataki Yanga ijulikane kwa matokeo pekee, bali pia kwa ubora na namna inavyocheza.

"Tunataka kucheza mpira wa possession, ku-press juu na kurejesha mpira haraka tunapoupoteza. Hatutaki kuwa timu ya kushinda tu, tunataka kuwa timu inayotambulika kwa style yake."

MAJERUHI NI CHANGAMOTO, LAKINI UBORA WA KIKOSI UPO

Fadlu amekiri kuwa kikosi cha Yanga kina wachezaji wenye ubora katika kila nafasi, lakini changamoto ya majeruhi imekuwa moja ya mambo yanayohitaji kufanyiwa kazi.

Amesema kipaumbele chake cha kwanza ni kujenga mfumo wake ili mashabiki wa Yanga waanze kuona mabadiliko ya kiuchezaji.

"Kikosi kina quality katika kila nafasi, lakini kuna majeruhi wengi. Kazi yangu ya kwanza ni kujenga style ambayo mashabiki wataijivunia na kuifurahia tena."

MALENGO SASA NI KUTIKISA AFRIKA

Kocha huyo ameweka wazi kuwa matarajio yake hayaishii kwenye mafanikio ya ndani pekee, bali anataka Yanga iweze kuwa na ushindani mkubwa katika michuano ya kimataifa.

Akizungumzia ushindani wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Fadlu amekiri kuwa kundi walilopo ni gumu na linaweza kutajwa kuwa kundi la kifo (Group of Death), lakini bado anaamini hakuna kisichowezekana katika soka.

Amesema:

"Hii ni era mpya. Hatutaki mafanikio ya ndani tu, tunataka mafanikio Afrika pia. Kundi la Champions League ni Group of Death, lakini everything is possible."

Yanga SC Stories

Goals : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL (FT)
Goals : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
FT : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL
FT : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL
11h ago
READ MORE β†’
Kikosi : JKT Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20
Kikosi : JKT Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20
14h ago
READ MORE β†’
Mudathir amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Mudathir amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Dladla awaaga Wananchi
Dladla awaaga Wananchi
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Polisi Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20
Matchday; Polisi Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yawasili Moshi tayari kuikabili Polisi Tanzania
Yanga yawasili Moshi tayari kuikabili Polisi Tanzania
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yakamilisha maandalizi tayari kuifuata Polisi Tanzania
Yanga yakamilisha maandalizi tayari kuifuata Polisi Tanzania
1d ago
READ MORE β†’
Dikgacoi atamba Yanga ipo tayari kuivaa Polisi Tanzania
Dikgacoi atamba Yanga ipo tayari kuivaa Polisi Tanzania
1d ago
READ MORE β†’