Uongozi wa klabu ya Yanga umethibitisha kuwa kiungo Maxi Nzengeli anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa wiki sita akiuguza majeraha ya goti.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema baada ya uchunguzi wa changamoto inayomsumbua, Maxi atahitaji kuwa nje kwa wiki sita kupona.
Akizungumzia hali za wachezaji wengine waliokuwa majeruhi, Kamwe amesema mlinda lango Hussein Masalanga nae anaendelea kukosekana wakati Duke Abuya na Yao Kouassi wakirejea kikamilifu.
Abuya na Yao jana walianza rasmi kushiriki mazeozi ya timu na wachezaji wengine ikiwa ni dalili ya urejeo wao kikamilifu.
Ni wazi sasa Maxi atakosa mechi zote ztakazopigwa mwishoni mwa mwezi huu kuanzia mchezo wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania na mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa dhidi ya MC Alger.