Inaelezwa licha ya kufikia makubaliano ya awali kumuajiri kocha Sead Ramovic, dili hilo limevunjika rasmi baada ya kocha huyo kuweka masharti mapya juu ya makubaliano ya awali.
Taarifa za uhakika kutoka chanzo cha kuaminika ni kuwa Ramovic alipata ofa nyingine kubwa zaidi ambapo aliutaka uongozi wa Yanga kuboresha dau lao ili aweze kutua nchini.
Hata hivyo Yanga haikuwa tayari kuboresha tena dau zaidi ya makubaliano waliyokuwa wamefikia awali.
Baada ya mpango huo kukwama Yanga imerejea kwa kocha Fadlu Davids ambaye alikuwa miongoni mwa machaguo ambayo Yanga ilikuwa nayo mezani.
Kocha huyo ameridhia kutua Yanga na pengine utambulisho wake unaweza kufanyika wakati wowote.
Fadlu ni kocha mwenye uzoefu na ligi ya Tanzania Bara akiinoa klabu ya Simba msimu wa 2024/25 na mwanzoni mw a2025/26 kabla ya kujiunga ya Raja CA.