FT : Yanga 4-0 Kagera Sugar, NC PL, Nov 1

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2h ago
FT : Yanga 4-0 Kagera Sugar, NC PL, Nov 1

Shoo ya kibabe kutoka kwa Wananchi imeshuhudiwa uwanja wa KMC Complex Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar.

Wakicheza soka la kasi, wakifanya pressing iliyowapa wakati mgumu Kagera Sugar kujenga mashambulizi kutoka chini, mabingwa hao watetezi wa ligi kuu walionyesha dhamra ya kuzihitaji alama tatu mapema tu pale Peter Shalulile alipoweka mpira kambani mapema bao lililokataliwa na FVS akiwa eneo la kuotea.

Hata hivyo muda mfupi baadae dakika ya 26 Shalulile alifunga bao jingine ambalo FVS walilikubali akimalizia krosi ya Maxi Nzengeli.

Dakika sita tu baadae zikawarejesha tena Kagera Sugar kuanza mpira katikati ya uwanja kwa mara nyingine baada ya Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' kufunga bao la pili akimalizia pasi mahiri kutoka kwa Stephane Aziz Ki.

Yanga ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0. Kipindi cha pili alikuwa ni Ibrahim Toure 'super sub' aliyeongeza mabao mawili dakika za lala salama.

Bao la tatu alilifunga dakika ya 87 kwa kichwa akimalizia krosi ya Zimbwe Jr kabla ya kufunga bao la 'kideoni' dakika za majeruhi baada ya kupokea krosi kutoka kwa Clement Mzize.

Ni ushindi ulioirejesha Yanga katika nafasi ya pili ikiwa ni mechi ya pili Wananchi wanashinda baada ya kipindi kigumu.

Β 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Highlights : Yanga 4-0 Kagera Sugar, NBC PL (FT)
Highlights : Yanga 4-0 Kagera Sugar, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Kagera Sugar, NBC PL, Nov 1
Kikosi : Yanga vs Kagera Sugar, NBC PL, Nov 1
6h ago
READ MORE β†’
Matchday : Yanga vs Kagera Sugar, NBC PL, Nov 1
Matchday : Yanga vs Kagera Sugar, NBC PL, Nov 1
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumapili, Novemba 01 2026
Magazeti ya leo Jumapili, Novemba 01 2026
17h ago
READ MORE β†’
Mzize arejeshwa kikosi cha Stars
Mzize arejeshwa kikosi cha Stars
1d ago
READ MORE β†’
Zimbwe Jr atuma ujumbe mzito Kagera Sugar, asema Yanga haijaridhishwa na nafasi ilipo
Zimbwe Jr atuma ujumbe mzito Kagera Sugar, asema Yanga haijaridhishwa na nafasi ilipo
1d ago
READ MORE β†’
Dladla atabiri mechi ngumu dhidi ya Kagera Sugar, ataka Wananchi kujitokeza kwa wingi
Dladla atabiri mechi ngumu dhidi ya Kagera Sugar, ataka Wananchi kujitokeza kwa wingi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumamosi, Oktoba 31 2026
Magazeti ya leo Jumamosi, Oktoba 31 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga vs Kagera Sugar ni Jumapili hii, hivi hapa viingilio
Yanga vs Kagera Sugar ni Jumapili hii, hivi hapa viingilio
2d ago
READ MORE β†’
Nini matarajio urejeo wa pili wa Ramovic?
Nini matarajio urejeo wa pili wa Ramovic?
2d ago
READ MORE β†’