Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga, wamewekwa katika Pot 2 kuelekea droo ya hatua ya makundi ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika (CAF Champions League) inayofanyika leo.
Hatua hiyo inamaanisha kuwa miamba hiyo ya Jangwani haitakutana na watani zao Simba SC, ambao pia wamepangwa katika chungu hicho kimoja.
Mbali na Simba, Yanga pia haitapangwa kundi moja na timu za Al Hilal ya Sudan pamoja na Petro de Luanda ya Angola zilizopo Pot 2.
Kwa mujibu wa taratibu za CAF, kila kundi litajumuisha timu nne, ambapo Yanga itapangiwa mpinzani mmoja kutoka Pot 1, mmoja Pot 3, na mmoja kutoka Pot 4.
Wapinzani wa Yanga wanaoweza kupangwa nao ni kama ifuatavyo:
Chungu cha Kwanza (Pot 1); Yanga itakutana na mbabe mmoja kati ya hawa: Esperance de Tunis (Tunisia), RS Berkane (Morocco), Zamalek SC (Misri) na Pyramids FC (Misri)
Chungu cha Tatu (Pot 3); Katika chungu hiki, Yanga inaweza kupangiwa timu moja kati ya zifuatazo: Orlando Pirates (Afrika Kusini), MC Alger (Algeria), Horoya AC (Guinea), FC Nouadhibou (Mauritania).
Chungu cha Nne (Pot 4); Hapa kuna uwezekano wa kukutana na: Club Africain (Tunisia), MAS de Fes (Morocco), Wiliete SC (Angola), Colombe Sportive (Cameroon)