Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera 'amedokeza' idadi ya wachezaji ambao wamesajiliwa na timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao na michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Yanga itaanza kujifua keshokutwa Jumatatu kujiandaa na mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Gor Mahia.
Zahera tayari amewasili nchini kuongoza mazoezi hayo.
Kwenye mahojiano yake na moja ya redio maarufu nchini, Zahera amesema kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuwa na mabadiliko kiasi.
Zahera amesema wamekusudia kusajili wachezaji hadi saba wapya ambao ana uhakika wataongeza nguvu katika kikosi cha Yanga.
Amesema miongoni mwao wapo wachezaji wa Kimataifa kutoka nchi za Zambia, Congo Brazzaville, DRC na Nigeria.

ADVERTISE HERE