Kikosi cha Yanga kimerejea salama jijini Dar es salaam wakitokea Arusha ambako jana walilazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya TRA United katika mchezo wa ligi kuu ya NBC.
Matokeo ya mchezo huo yalipelekea ajira ya kocha mkuu Manqoba Mngqithi kuota mbawa.


Wakati uongozi wa Yanga ukiendelea na mchakato wa kusaka kocha mpya, Kocha Msaidizi Simo Dladla anatarajiwa kukiongoza kikosi kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa Fc utakaopigwa Jumanne dimba la KMC Complex.
Dladla ni kocha mwenye uzoefu mkubwa akizinoa klabu kadhaa za ligi kuu ya Afrika Kusini kama Amazulu na Maritzburg.
ADVERTISE HERE