Baada ya kudondosha alama mbili mkoani Arusha, presha imezidi kuongezeka kwa kocha Manqoba Mngqithi na benchi la ufundi. Saa 24 zijazo huenda zikawa ngumu kwake 'kibarua' chake kikiwa hatarini.
Yanga imekosa ushindi katika mechi mbili zilizopita za ligi huku ikionyesha kiwango cha chini. Leo katika mchezo dhidi ya TRA United timu haikuonekana kuwa na ari ya kusaka ushindi, ile kasi ya Yanga iliyozoeleka haikuonekana.
Taarifa za ndani zimebainisha kuwa tayari mazungumzo baina ya pande mbili yameanza huku uongozi pia ukianza msako wa mbadala wake.
Jina la kocha Sead Ramovic 'Gusa Achia Twende Kwao' limerejea tena mezani huku pia kukiwa na taarifa za mawasiliana na kocha Fadlu Davids ambaye awali ndiye aliyehitajika kabla ya ujio wa Manqoba.
Licha ya uongozi wa Yanga awali kuweka msimamo kuendelea kumuamini Manqoba katika nafasi yake, lakini wakati huu ni wazi msimamo huo unaweza usiwepo kutokana na mwenendo wa timu.